MALENGO YA CHAMA
Madhumuni Yetu
01
Kutatua matatizo na changamoto mbalimbali
Mfano
- Kifo- pale ambapo Mtanzania ambaye ni mwanachama wa UTU anafariki. Chama kusimamia maandalizi na sheria zote zinazohusu marehemu na kusafirisha mwili nyumbani tukishirikiana na ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani ,na familia na ndugu jamaa wa Marehemu.
- Kesi-Mtanzania anaweza akaja hapa na akapata matatizo ya kisheria,hivo chama kita simama naye kuhakikisha Mtanzania anapata haki zake zote.
- Taarifa- Kuwezesha Mtanzania kupata majibu ya maswali ambayo mtu atakua anahitiji kujua ya hapa Ujerumani ili aweze ishi kwa ndoto zake.
- Masomo
- Sheria
- Kazi
- Biashara
02
Project
Kupitia chama hiki (diaspora) unaweza pata mtandao (connection nyingi) mkubwa kupitia ofa nyingi ambazo nchi yetu inatoa, na kutupa kipao mbele sisi Diaspora ,kufanya maendeleo nyumbani.
03
Kukutanisha Watanzania
Kupitia sherehe za kitaifa na kijamii hapa Ujerumani ili kudumisha mila na desturi za Tanzania. Pia kuwaunganisha Watanzania nchini Ujerumani kwa kuhakikisha mshikamano wa kudumu na ushirikiano wenye tija miongoni mwao.
04
Kuitambulisha Tanzania
Katika ulimwengu wa Ujerumani kwa kukuza taswira yake chanya.
05
Kuimarisha na kushawishi ushiriki wa wanadiaspora
Katika kusaidia miradi ya maendeleo ya kijamii nchini Tanzania